"Tulipo endelea, tuliwaona maelfu ya watu kwenye mateso,Wakati roho inapo mwona Bwana, zilijitahidi kumfikia kwa mikono isiyo na ngozi.Nilimwona mwanamke aliye anza kupiga makelele alipo mwona Bwana Yesu. Alilia, "Bwana tafadhali nirehemu! nitoe mahali hapa!" Alikuwa akiteseka sana na aliunyoosha mkono wake kwa Bwana.Aliendelea kumwomba Bwana amtoe eneo lile hata kwa sekundr moja.
Alikuwa yuu uchi kabisa na alifunikwa na tope. Nywele zake zilikuwa ni chafu na minyoo ilikuwa ikijongea mwilini mwake .Alijaribu kuiondoakwa mikono yake lakini kila alipo mwondoa mmoja mingine ilijizisha zaidi.Minyoo ilikuwa na urefu karibu inchi 6-8.Neno la Bwana linasema katika Marko 9:44, "Ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki."
Ilikuwa ni ya kutisha sana kumwona mwanamke huyu na kusikia kilio chake kwa jinsi minyoo ile kwa hasira ilivyo kuwa inaila nyama za mama huyu. Kulikuwepo na bango la chuma lililo kifuani mwake ambalo lisingeweza kuharibiwa na moto.
Lilisomeka , "Nipo hapa kwa ajili ya Uzinzi." Kwa jinsi ile ile ya dhambi yake, mwanamke huyu alilazimishwa kufanya uzinzi kuzimu na nyoka wa kutisha mnene..Nyoka huyu alikuwa na miiba mikubwa kuuzunguka mwili wake, ni kama ya uerfu wa inchi 6-8 hivi.Nyoka humwingia mama hyu sehemu zake za siri na kusafiri hadi mwilini mwale hadi kwenye koromeo lake. Nyoka alipo mwingilia hivi, alianza kulia kwa makelele .
Alimwomba Bwana kwa nguvu sana amtoe eneo lile, "Bwana, nipo hapa kwa ajili ya uzinzi, nimekuwepo hapa kwa miaka 7, tangu UKIMWI ulipo niua. Nilikuwa na wapenzi sita6, na nipo hapa kwa ajili ya uzinzi." Kule kuzimu alitakiwa kuirudia dhambi yake tena na tena.
Hakuna kupumzika usiku na mchana, akiteseka kwa jinsi ile ile kila mara. Alijaribu kuunyoosha mkono wake kwa Bwana, lakini Bwana alimwambi, "Blanca, kwako tayari umechelewa. Minyoo itakuwa ni kitanda chako, na minyoo itakufunika." (Isaya 14:11) Wakati Bwana alipo sema maneno hayo, blanketi la moto lilimfunika, na siku mwona tena."
Home »
» Zinaa mbaya soma ushuhuda wa binti huyu toka kuzimu