Pindi nilipojiunga chuo kimoja hapa bongo, nilikuwa kijana mwembamba, tall HB fulani hivi. Nikakutana na msichana moja , ngoja nimuite Angel. Angel alikuwa ni mzuri na yupo classy. Tukawa marafiki, kiukweli alikuwa ni msichana wa kwanza kuzungumza naye darasani. Kwa hiyo nikajaribu kuweka mambo sawa na Angel. Tulitoka out, tulipigiana simu, nilikaa jirani naye darasani.

Nikaweza fanikiwa kuwekeana naye miadi ya mtoko katika siku ambayo wote tulipaswa turudi majumbani. Nilifurahi sana. Naliazima kwa rafiki yangu saa nzuri kufanikisha reallry swaga. Baada ya matayarisho nilikuwa na furaha sana pamoja na marafiki zangu nao walikuwa na furaha. Nikampigia simu Angel, akupokea simu. Nakampigia mara nyingi akupokea mara lisaa, masaa hakupokea. Baada ya masaa kupita akanipigia simu tayari ameshafika nyumbani kwao

Nilihuzunika sana kupita kiasi. Ilikwa ni siku ya uzuni sana kwangu, sito weza sahau siku ile. Marafiki zangu walinicheka sana kupita maelezo. Baadae kidogo niliwachukuwa marafiki zangu tukaenda kuspend pesa niliyotaka kuspend na Angel.


Baada ya uzoefu nilibadilisha namna nyingine kabisa ya maisha ya chuo katika uwepo wa macho ya Angel. Nikaacha kumpigia simu, Pesa ambayo nilikuwa namuassist nikawa natupia pamba na swagg zote. Nikawa kama nimezaliwa sehemu ambayo Angel hayupo. Nikawa marafiki na ma hot girls darasanai, punde nikatambua Angel ajisikii vizuri. Nikawa popular ndani ya darasa na chuoni kote, nikawa ni kijana ambaye wasichana wananipenda, nilikuwa mchangafu na wakujutuma katika taaluma. Nikaanza kujifanya nipo busy sana na mambo yangu. Nikawa rafiki wa marafiki zake Angel, ukweli walinipenda. Nikawa namuona Angel akiwa na sura ya udhuni. Nikawa na msalimu kwa tabasamu la kisexy.


Angel ikafikia stage akanipigia simu siku moja na akaniomba msamaha, aliniambia amenimiss. Nilijisikia vizuri ila sikurudi nyuma, nikaendelea na maisha yangu. Tukawa marafiki tena lakini sikurudi nyuma kama siku zile. Akajitambua kwamba mda ule ndio alikuwa amepoteza japokuwa nilikuwa na opportunity ya kumpata lakini nikapotezea. Tukabaki hivyo hivyo mpaka siku tumegraduate’


Storry yangu hapo juu ni fundisho kwa vijana: Kuwa na uwezo wa kucontrol emotion zako, kuwa kijana mwenye kujali less about girls na zaidi ujijali wewe mwenyewe. Ukiweza hivyo, hutaweza kuumizwa for life