Home » » Ngono ya mdomo ni hatari

Ngono ya mdomo ni hatari

Written By Unknown on Friday, February 21, 2014 | 12:13 AM


Namna mdomo unavyoharibika kutokana na ngono kufanywa kwa kutumia mdomo. 



  • Baadhi ya watu ambao wanakumbwa na ugonjwa huu shingo huvimba kama hivi. Hata hivyo wapo wenye kuvimba hivi lakini si kwa sababu walifanya ngono kwa kutumia mdomo, isipokuwa yaweza kuwa ni sababu nyingine zikiwemo kurithi. 
  • Wataalamu wa masuala ya afya wanashauri kwamba ni muhimu sana watu wakaachana kabisa na tabia hii kutokana na ukweli kwamba siyo tu kwamba ni hatari kwa afya, pia ni sawa na kujiua mwenyewe, kwani kitendo hicho kinachangia magonjwa mengi.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,
 pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa  ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti  huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747  na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni  kuwavutia wapenzi wao katika  kushiriki ngono.
Vijana  wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari  Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya  koo ni  ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume  nchini, ikiongozwa na ile ya  ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya  koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na  umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze  kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” anasema  Dk Kahesa na kuongeza.
Share this article :
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Smasher Tz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger