
IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego wa kujiuza na makachero wa OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na maisha ya presha.
Baby Madaha.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha
alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata
kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.

Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi na nane za Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ambapo alipatana bei ya kutoa uroda kwa ‘mfanyabiasha’ wa madini kutoka jijini Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Mike – kumbe ulikuwa mtego.