Mwanamke, nakuita mwanamke wewe ni kipofuuu? Usiniambie siyo mimi sijakuita jina lako nimeita umbile lako wewe mwanamke ni kipofu? Simaanishi upofu wa macho, mwanamke unaona vizuri sana ndiyo maana unaenda kujiuza lakini hujijui kama wewe ni kipofu.

Jaman, nimepita mitaa ya Dar muda huu mingi na usafiri wangu binafsi nijionee dunia inakwendaje, nilichokiona dunia imeharibika. Mwanamke nakuhurumia sana, uendekezaji wa umalaya huo na kujiuza je macho yako yanaona hapo baada ya miaka 30-40 mbele utakapokuwa mzee?

Mwanamke unajiuza sasa kwa pesa hata kama unapewa laki moja kwa siku lakini jicho lako linaona baada ya miaka kadhaa uzee utakapokunyemelea?

Hii nchi baada ya miaka 30 na kuendelea itakuwa na matatizo makubwa sana, vifo vitakuwa vya kawaida atakayekuwa amefungua kampuni ya kuzika maiti anaweza kuuza sana nakuwa bilionea. Huyu mwanamke kipofu anyejiuza aliyeboea kwenye biashara ya ngono bila kujua hapo baadaye atakuja kupukutika kama maua. Usiniambie na mwanaume je? Somo la leo linakuhusu wewe mwanamke, mwanaume siku nyingi.

Ninalia sana na niliyoyaona mtaani!