Na BARAKA MBOLEMBOLE
NI
mataifa machache sana yenye historia ya soka kama Uruguay ' The Sky
Blue One'. IKiwa ni nchi yenye wakazi wasizidi millioni nne Uruguay
inajivunia kuwa moja ya mataifa yenye mataji mengi ya kimataifa duniani.
Imetwaa ubingwa wa kombe la dunia mara mbili, 1930, na 1950, pia
wanaongoza kwa kutwaa ubingwa wa Amerika ya Kusini mara nyingi zaidi,
mara 15, huku ubingwa wao wa mwisho wakitwaa mwaka 2011 nchini
Argentina.
Mabingwa
hao wa kwanza wa dunia, tayari wamecheza michezo 47 ya fainali za
kombe la dunia, wakiwa wamepata ushindi mara 18, kutoa sare mara 12 na
kupoteza michezo 17, wamefunga mabao 76 na kuruhu nyavu zao mara 65.
Walimaliza katika nafasi ya nne katika fainali zilizopita, WOZA 2010, na
sasa wamefuzu kwa fainali zao za 12 kati ya 20.
Kiwango
cha sasa cha nchi ya Costa Rica kinaweza kufanya kundi hilo kuhesabika
kama ni moja ya makundi magumu zaidi, kwani wawakilishi wa Ulaya,
England na Italia walifanya vibaya katika fainali zilizopita. England
iliishia hatua ya 16 bora na Italia ilishindwa hata kuvuka hatua ya
makundi.
Mabingwa
hao mara nne, ' Azzurri' ni moja ya mataifa mawili ambayo yanashikilia
rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo sambamba na Brazil,
Italia ilitwaa katika miaka ya 1934 na 1938, wakarudia tena katika miaka
ya 1982 na 2006.Wamefuzu kwa mara ya 13 mfululizo kati ya mara 17
walizowahi kufuzu. Hii ni timu ya kombe la dunia. WAmefuzu mbele ya
mataifa ya Denmark, Czech Republic, Bulgaria, Armenia na Malta,
wakishinda michezo sita na sare nne kati ya michezo 10 waliyocheza.
Kikosi
hicho kiliifunga England katika robo fainali ya michuano ya Euro 2012
na hatimaye kufika fainali wakati huo. Imeshacheza jumla ya michezo b3,
wakishinda michezo 45, sare katika michezo 21, na wamepoteza mara 17,
wamefunga mabao 130 na wameruhusu mabao 78. Italia na Uruguay zinaweza
kuvuka kundi hili na kuziacha nje England na Costa Rica.
England
' The Three lions' wamefuzu tena kwa fainali za kombe la dunia. NI moja
ya timu maarufu sana katika michuano hiyo japo huwa haifanyi vizuri.
Mafanikio yao ya mwisho ni katika fainali za mwaka 1990 walipofanikiwa
kufika hadi hatua ya nusu fainali, walishindwa kufuzu kwa fainali za
mwaka 1994 na wakaondolewa katika hatua ya robo fainali katika fainali
za miaka ya 2002, 2006, na wakaishia hatua ya mtoano mwaka 2010.
Wamewahi
kucheza michezo 59 katika fainali 13 walizopita miaka ya nyuma,
wameshinda mara 26 tu, sare wametoa mara 19 na wamefungwa michezo 14. Ni
moja ya timu zenye uhaba wa mabao katika michuano hiyo, wakiwa
wamefunga mabao 77 na kuruhusu mabao 52 ni wastani wa chini katika
ufungaji na uzuiaji katika kombe la dunia. Costa Rica wanatajwa kama
vibonde katika kundi hili wamefuzu kwa fainali zao za nne. Wamewahi
kuishia hatua ya 16 bora katika fainali za mwaka 1990 na wamewahi
kuishia hatua ya makundi katika miaka ya 2002 na 2006. WAmecheza michezo
10 ya fainali za kombe la dunia, wameshinda michezo mitatu, wametoa
sare mchezo mmoja na wamepoteza michezo sita. Hii ni ratiba ya mechi za
kundi hili.
June 14 Fortaleza, 2000:
Uruguay v Costa Rica
Uruguay v Costa Rica
June 15 Manaus, 0200:
England v Italy
England v Italy
June 19 Sao Paulo, 2000:
Uruguay v England
Uruguay v England
June 20 Recife, 1700:
Italy v Costa Rica
June 24 Natal, 1700:
Italy v Uruguay