Popular Posts

Blog Archive

Latest Post

AFANDE KASEMA ATANIBAMBIKIA KESI

Written By Unknown on Thursday, April 3, 2014 | 10:00 AM



Jamaa kasimamishwa na trafiki kwa kosa la mwendo mkali;
TRAFIKI: Mheshimiwa unajua ulikuwa unakimbia spidi kali sana?
DREVA: Sasa leseni sina, gari niliiba, halafu chini ya kiti nina pisto ya wizi unadhani ntaendesha polepole
TRAFIKI: Mungu wangu kumbe we jambazi?
DREVA: Si jambazi tu, pia huwa nauza viungo vya binadamu, kwenye buti kuna vipande vya miili vya watu....trafiki haraka akaita msaada wa polisi wenzie waliofika baada ya muda mchache wakiogozwa na afande mkubwa
AFANDE: Askari vipi tena hapa?
TRAFIKI: Afande nimelikamata jambazi sugu. Halina leseni, gari ni la wizi, limeficha pisto chini ya kiti na kwenye buti kuna vipande vya miili ya binadamu.
AFANDE: Leseni yako iwapi?
DREVA : Hii hapa afande na kadi ya gari hii hapa
AFANDE: Askari mbona leseni iko safi, na gari ni lake sio la wizi? Hebu sachini gari kama kuna hivyo vitu alivyoviona askari....gari likasachiwa lilikuwa safi
DEREVA: Afande askari kaninyanyasa sana huyu kasema yote hayo asiponibambika atasema nilikuwa naenda mwendo kasi
AFANDE: Mheshimiwa wewe nenda, jeshi litajua namna ya kushughulika na huyu askari aliyekusumbua

KUNA BAR SINZA WANATOA WAPENZI BURE




MWANAKIJIJI 1: Aise nataka kwenda Dar
MWANAKIJIJI 2: Lazima ufike Sinza kuna baa inaitwa SHKAMOO
MWANAKIJIJI 1: Kwanini?
MWANAKIJIJI 2: Hapo ukiingia wanakupa kinywaji bure, halafu unapotoka unapewa mpenzi bure
MWANAKIJIJI 1: Dah huko lazima niende, we uliwahi kufika huko?
MWANAKIJIJI 2: Hapana lakini mke wangu kila akienda Dar lazima afike hapo

BOSI WAKO TAAHIRA

Written By Unknown on Wednesday, April 2, 2014 | 1:16 PM




Kijana kaajiriwa kuuza duka, bosi wake akamwacha anaendelea na shughuli, masaa machache baadae bosi akarudi akamkuta kijana anabishana vikali na mteja. Bosi akafika na kuanza kumtukana yule kijana;
BOSI: Wewe pumbavu vipi? katika biashara mteja ni mfalme, acha upumbavu wa kubishana na mteja atakachosema mteja ndicho hakuna vingine na uelewe hilo kuanzia leo. Haya mnabishana nini hapa?
KIJANA: Bosi huyu mteja alikuja hapa akaanza kunambia Bosi wako taahira

CHONDECHONDE UKIKAMATWA NA POLISI USITOE MAJIBU HAYA





Tafadhali ukiwa unaendesha gari ukasimamishwa na polisi tafadhali jizuie usitumie majibu yafuatayo:
- i. Hebu nishikie konyagi yangu nikutolee leseni
- ii. Nilitaka na mimi kuwa polisi nikaona huu ufala
- iii.Unajua mshahara wako unatoka kwangu mimi mlipa kodi?
- iv. Bosi wako mwenyewe tulisoma nae praimari alikuwa mjingamjinga
- v. Umejuaje nimekunywa, au na wewe mdau?
vi. Jela zimetengenezwa kwa ajili yetu



SAMAHANI BABY NILIDHANI UNA MIMBA






MDADA: Halloo Baby, Mpenzi kuna kitu cha muhimu naomba nikuone tuongee
MKAKA: Nini tena usinambie una mimba
MDADA: Baby kwa vyovyote vile nyumbani watanifukuza wakishasikia nina mimba yako
MKAKA: Huo upumbavu sitaki kuusikia si nilikuwa ninakupa fedha ukanunue vidonge vya majira?
MDADA: (Huku akilia) Ndio honey lakini imetokea kama ajali, samahani baby
MKAKA: Samahani baby kamwambie baba yako, sitaki kuiona sura yako nyumbani kwangu tena
MDADA: Baby please nielewe
MKAKA: Hata ukiniona barabarani usinisalimie mwendawazimu mkubwa.
MDADA: Lohhhh kumbe ndivyo ulivyo? Nashukuru Mungu sina mimba nilikuwa nakutest tu
MKAKA: Ahhhh si unajua baby panic ya kawaida hiyo, vipi uko wapi saa hizi nikupe mchemsho?
MDADA: Sikutaki wala sitaki mchemsho wako wewe huna ubinadamu
MKAKA: Achana na hayo, samahani baby
MDADA: Samahani kamwambie mama yako

JE UNATAKA KUJA DAR ES SALAAM? ZIJUE STAILI ZA KUVUKA BARABARA KWANZA




Kwa kweli blog hii asubuhi hii imeona itoe ushauri kwa ndugu wananchi ambao wanaopanga kuja katika jiji la Dar es Salaam aidha kutembea au kuhamia au hata kuja kufanya kazi ya uhauzgelo. (Siku hizi blog hii imegundua kuna mahauzgelo kadhaa wanaoisoma ili kuongeza akili.)
Ndugu mwananchi, ukifika Dar katika moja ya mambo ambayo yatakuchanganya ni namna ya kuvuka barabara. Kwanza kuna barabara za aina nyingi sana, kwa mfano kuna nyembamba za njia moja, ziko nyingine ni njia mbili, kuna hata moja inatoka Moroko hadi Mwenge ambayo hata wanasayansi wa kimataifa wameshindwa kujua kama ni ya njia 3,4,5 au 6. Ni hatari sana kuvuka barabara hii ya Mwenge Moroko.
Ukifika Dar kabla hujavuka barabara kwanza angalia kushoto, kisha kulia, kisha kushoto, kisha kulia chonde chonde usianze kuvuka hata kama hujaona kitu pia tumia masikio kusikiliza kama kuna kitu kina kuja, kuna hawa jamaa wa bodaboda na bajaj, huwa wanazuka kama majini ghafla unawakuta wako mguuni kwako ni muhimu sana kuhakikisha hawako jirani, bado usinyanyue mguu kuvuka angalia juu kwanza, hapa Dar kumekuwa na mchezo wa kujenga ghorofa kwa kutumia mchanga wa baharini ili kupunguza matumizi, ghorofa kadhaa zimekwisha dondokea vichwani mwa watu hapa mjini, hivyo angalia juu pia kucheki kama ghorofa la jirani liko poa? Wakati huohuo angalia nyuma, mji una vibaka huu balaa. Kama una mtindo wa kizamani wa kuweka pochi mfuko wa nyuma ni muhimu uwe na jicho huko usije ukavuka barabara kumbe wenzio wamchukua pochi. Kama uko mitaa ya Tandika, Manzese, Kinondoni Mkwajuni wakati unataka kuvuka ukisikiaa ghafla mtu anakwambia "mdudu huyo, mdudu huyo", we endelea kuvuka usiogope hao ni matapeli wanataka kukuchanganya wakuibie simu. Baada ya hapo kama kila kitu kiko poa, Mungu akusaidie anza kuvuka huku ukikwepa magari kwa staili ya Rambo anavyokwepa risasi. Hii staili ya kukwepa risasi inaweza kukusaidia sana maana pia unaweza kuwa unavuka barabara ukakuta kuna jamaa wameamua kutembeza risasi kwenye shughuli zao za ujambazi. Hata hivyo wanyalukolo wenzangu karibuni Dar

Je wajua athari za kuitana sweet , honey , baby katika mapenzi???




BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby!
Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine).
Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji.

HUTUMIKA WAPI HASA?
“Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.”
Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo. Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile, ila iwe inatambulika vizuri na anayetamkiwa.

ATHARI SASA!
Kwa upande mwingine kuna athari za kutumia maneno hayo. Zama hizi, maneno hayo yanaonekana ya kawaida tu. Mtu yeyote anaweza kumuita yeyote mpenzi, honey, baby n.k. Hapo ndipo kwenye tatizo lenyewe.
Kwa ujumla wanawake ndiyo wanaongoza zaidi kuitana majina hayo. Wakati mwingine huenda mbali zaidi na kuwaita hata wanaume majina hayo ya kimapenzi. Si rahisi kuona athari zake kwa haraka na moja kwa moja, lakini zipo na wengi zimewasababishia matatizo. Ngoja tuone..

HUPUNGUZA THAMANI
Kama nilivyotangulia kusema awali, maneno
niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.
Kama unaweza kumwita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.

HUKARIBISHA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Veronica, mfanyakazi wa saluni moja ya kiume iliyopo Sinza, Dar alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni. Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kumfurahisha mteja na wakati mwingine kumfanya akupe tipu baada ya kumaliza kazi.
“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.
“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.
“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”
Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu zangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka sana – hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzi.
Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo?

ANGALIA TOFAUTI
Rafiki zangu, kati ya maneno niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano lakini wawe na undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.
Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi. Umenipata? Akili za kuambiwa, changanya na zako kisha unazifanyia kazi! Chukua kinachokufaa
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Smasher Tz - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger